UZALISHAJI UPYA WA MAFUTA

UZALISHAJI UPYA WA MAFUTA YA TRANSFOMA

Hali ya kizuizi cha karatasi na mzunguko wa sumaku wa transfoma ndizo ambazo huamua urefu wa huduma yake. Hakuna mipaka ya urefu wa huduma wa sumaku ila kizuizi cha karatasi kinaweza kupatwa na mkazo na kuisha baada ya muda; hii inafanya hali ya kizuizi cha karatasi kuwa ndiyo muhimu zaidi katika kuhakikisha huduma ya muda mrefu ya transfoma. Kwa kawaida, kizuizi cha karatasi huzeeka baada ya muda mrefu lakini mchakato huu unaweza kuharakishwa kwa kiwango kikubwa na joto, oksijeni, maji, na vitu vingine vinavyotokana na kuchanganyikana kwa oksijeni na mafuta kwenye transfoma. Bidhaa hizi hukusanyika kwenye karatasi kadri muda unavyosonga.

UZALISHAJI UPYA WA MAFUTA NA USAFISHAJI WA KIZUIZI CHA KARATASI

Kama tulivyosema hapo awali, kizuizi cha karatasi hukusanya bidhaa zinazotolewa na mafuta yanapozeeka na kutumika kama kichujaji cha mafuta. Kubadilisha mafuta kwenye transfoma sio suluhisho kamili: mara tu transfoma inapojazwa na mafuta mapya, uchafu uliokusanyika kwenye kizuizi kile huoshwa na kuchanganyika na mafuta. Uchafu huu huzidisha mchanganyiko wa oksijeni na mafuta na kutengeneza uchafu mwingine kwenye kizuizi cha karatasi, na mzunguko unajirudia tena na tena na tena. Tunapozingatia kurefusha huduma ya transfoma, kubadilisha mafuta sio suluhisho lenye faida ya mia kwa mia. Wala mchakato wa kuyatoa mafuta kutoka kwenye transfoma, kuyazalisha upya, na kuyarudisha tena kwenye tangi la transfoma: matokeo ya mwisho ni sawa na yale ya kubadilisha mafuta tu. Faida tu ni kuwa gharama yake ina nafuu kidogo. Jambo hili linaweza kutatuliwa, kwa kiasi fulani, wakati wa ubadilishaji wa mafuta kwenye transfoma. Kusafisha karatasi na mafuta safi kunaweza kutoa kiasi kikubwa cha uchafu ila uchafu unaokusanyika kutokana na machanganyiko wa oksijeni na mafuta ndani ya karatasi bado ni ngumu, au hata haziwezekani, kutolewa. Matumizi ya sabuni za kipekee husaidia ila zina gharimu pesa nyingi na pia huongeza muda unaohitajika kwenye mchakato huu. Kwa ufupi, kurekebisha transfoma na kuosha kizuizi cha karatasi kunaweza kugharimu kiasi cha fedha sawa na thuluthi ya bei ya kununua transfoma mpya.

VIFAA VYA UZALISHAJI UPYA WA MAFUTA

Kuna njia ufanisi na za bei nafuu zinazotatua matatizo yaliyotajwa hapoawali: viwanda vya uzalishaji upya wa mafuta za GlobeCore CMM-R. Mojawapo ya sifa zinazotenga mifumo hii yenye ufanisi wa hali ya juu ni kuwa zinaweza kusindika mafuta katika transfoma iliyo na mtiririko wa nguvu za sumaku. Uwezo huu huifanya mashine hii kuwa suluhisho bora la tatizo la matibabu ya kizuizi cha karatasi. Matumizi ya CMM-R huanza na kuunganishwa na transfoma iliyo na mtiririko wa nguvu za sumaku. Mafuta kutoka kwenye transfoma hupitia ndani ya kitengo hiki kwa usindikaji, bidhaa zinazotokana na mchanganyiko wa oksijeni na mafuta hutolewa, kwenye transfoma pamoja na mafuta ambayo hupitia michakato ya kuzalisha upya na utoaji wa hewa iliyopita kiasi. Baada ya usindikaji mafuta hurudishwa kwenye transfoma, kisha mchakato huu unarudiwa katika mizunguko kadhaa. Mafuta yaliyozalishwa upya huosha bidhaa zinazotokana na mchanganyiko wa oksijeni na mafuta kutoka kwenye kizuizi cha karatasi. Mchakato wa usafishaji huu unaboreshwa na mzunguko wa kasi, joto, na mtetemko wa transfoma yenye mtiririko wa nguvu za sumaku. Uchafu unapotolewa kwenye karatasi, unaingia kwenye mafuta, na kuzuiliwa kwenye kitengo cha ufyonzaji ambapo mafuta yanazalishwa upya na kutolewa hewa iliyopita kiasi. Kitengo hiki huwezesha uzalishaji upya na usafishaji wa mafuta ya transoma na vile vile usafishaji wa jumla wa kizuishi cha karatasi. CMM-R pia ina faida zifuatazo:
  • Kurefusha muda wa huduma ya transfoma
  • Usafishaji wa kizuizi na kukomesha kudhoofika kusikoweza kubadilika kunakosababishwa na bidhaa zinazotokana na mchanganyiko wa oksijeni na uchafu mwingine
  • Utendaji unaoendelea katika transfoma zenye mtiririko wa nguvu za sumaku.
  • Kitengo cha ufyonzaji cha Fuller’s Earth kinaweza kuwezeshwa tena na kutumika tena kwa hivyo kuondoa hofu za athari kimazingira
  • Upotezaji wa mafuta katika mchakato wa ufyonzaji unapunguzwa
  • Uzalishaji upya wa mafuta na matibabu ya kizuizi cha karatasi zinafanyika kwa wakati mmoja

MAFUTA YA TRANSFOMA

Mbali na kulinda karatasi iliyo kwenye transfoma na vifaa vingine vya kizuizi kwenye transfoma, mafuta yanatumika pia kama mtindo wa kupunguza joto kwenye transfoma, swichi za volteji ya kiwango cha juu, kebo za OF, na kapasita. Mafuta ya transfoma ni bidhaa ya usindikaji  wa mafuta ghafi. Kwa sababu sifa za mafuta ghafi hutofautiana kulingana na aina haswa ya ghafi (ujumla wa aina tofauti za kemikali), na vilevile sifa za madini ya mafuta ya transfoma. Ndani ya transfoma, mafuta hupitishwa michakato inayosababisha mchanganyiko wa oksijeni na mafuta na udhalili. Ubora na utendaji wa mafuta hupungua na kufanya mchanganyiko wa oksijeni na mafuta kipengee muhimu katika hali ya jumla ya transfoma na muda wa huduma yake kwa ujumla. Mafuta ya transfoma yanaweza kusindikwa: kuzalishwa upya na kusafishwa ili kutoa asidi, maji, na hewa, na uchafu mwingine kama vile lami, emboe, hidrokaboni zingine, sulfuri, na misombo mingine ya nitrojeni, n.k. Kuna njia nyingi za usindikaji  wa mafuta ya transfoma, ambazo zinaweza kugawanywa kwa viwango vifuatavyo: kimashine, kijoto, kimwili na kikemikali, na kikemikali tu. Za mwisho zina gharama ya juu na zinahitaji mifumo migumu, na hutumika tu ikiwa njia zingine rahisi hazikutoa mafanikio ya kuridhisha. Mchakato wa CMM-R ni rahisi na wenye ufanisi: hali ya mafuta yaliyo sindikwa huwa ni “nzuri kama ya mafuta mapya”, na ubora wake unalingana na vifungu vya viwango vya IEC 60296. Kwa kutumia mfumo huu kushughulikia suala la usafishaji wa mafuta na kizuizi cha karatasi kunaboresha ubora wa uzuizi kwenye transfoma, na kurefusha muda wake wa huduma pamoja na kupunguza urekebishaji unaotokana na shida zisizotarajiwa na muda mrefu wa kutotumia vifaa. Baada ya matibabu ya mafuta ya transfoma katika kiwanda cha GlobeCore СMM-R, ubora wake unalingana na mahitaji ya ubora ya kitaifa ya IEC 60296.

MIFUMO YA UZALISHAJI UPYA YA GLOBECORE

Masuala ya kimazingira yanaendelea kuleta wasiwasi kwenye usindikaji katika viwanda, na waekezaji wanaonekana kupendelea zaidi usindikaji unaohifadhi mazingira. Vitengo vya CMM-R vimeundwa kwa kuzingatia mazingira kwani vina uwezo wa kuwezesha bidhaa zinazotumika katika mchakato wa ufonzaji tena na tena, kabla kupoteza nguvu zake na kuhitaji kutupwa– kama uchafu safi wa madini. Kwa hakika, uwezeshaji tena huu huokoa pesa ambazo zingetumika kununua kifaa kipya cha kuwezesha ufyonzaji kila mara. Pia, inaondoa haja ya kununua mafuta mapya. Muda wa huduma wa transfoma unaongezeka kwa kwa kiwango cha miaka 20 hadi 30, ambayo pia huboresha usawa wa kimazingira wa teknolojia. GlobeCore ni mtengenezaji wa mifumo ya uzalishaji upya wa mafuta inayolingana na mahitaji ya waendeshaji wa transfoma, kuhudumia biashara na watengenezaji. Bidhaa hii ya kampuni inaleta sulushisho za usafishaji wa transfoma, turbini, mafuta ya viwandani na mahali kwingine kwa urahisi, utendaji wa hali ya juu, na viwanda vya urejelezaji halisi. Bidhaa hizi za kampuni hutumika bila kutoa  hewa chafu zozote zitakazodhuru mazingira na lina ubora wa kutumia nguvu ili kupunguza gharama ya utendaji.

MTENGENEZAJI

Globecore oil regeneration offices
GlobeCore

Leave your request